MrB - Uliyenijalia Lyrics
- Just In Faith

- Nov 26, 2021
- 1 min read
Bila shaka wewe, ni mungu wa kweli
Tena wewe waajabu, matendo yako yatisha
Watetemesha milima, miamba, kwa pumzi yako tu
Warejesha uhai, na afya, mifupa mikavu
Hivi basi nieleze, ni kipi usichokiweza
Kitu gani nilinganishe na mambo unayoyatenda
Fikra zako zanizidi umri, siwezi eleza
Vitabuni nikinakili siwezi maliza
Fikra zako zanizidi umri, siwezi eleza
Vitabuni nikinakili mie siwezi maliza
Kazi ya mikono yako Yesu, naishuhudia
Nitaimba sifa zako, Jehovah
Si kwa nguvu na uwezo nilionao
Si kwa hekima na maarifa niliyonayo
Si kwa nguvu na uwezo nilionao
Si kwa hekima na maarifa niliyonayo
Uliyenijalia, nitaimba sifa zako
Uliyenijalia, Jehovah
Uliyenijalia, Ni wewe bwana
Uliyenijalia, Jehovah
Uliyenijalia, nitaimba sifa zako
Uliyenijalia, Jehovah
Uliyenijalia, Ni wewe bwana
Uliyenijalia, Jehovah





Comments